Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Bahjat (ra), akitaja tajiriba ya watu wengi, amesema kuwa iwapo ndani ya moyo wa mtu itaingia nia ya kuswali Swala ya usiku, basi sababu za kumwamsha huandaliwa kwa njia mbalimbali.
Ayatollah Bahjat (ra):
"Jambo hili limethibitika kwa yakini, na watu wengi wamelisimulia, kwamba iwapo itaonekana bayana kuwa mtu anataka kuswali Swala ya usiku, basi huamshwa; aidha hugongewa mlango, au hutokea sauti fulani, au huitwa kwa jina lake, na kadhalika..."
Chanzo: Dar Mahzari-ye Bahjat, juzuu ya 3, uk. 188
Maoni yako